Tanzania yajiweka tayari kukabiliana na magonjwa ya milipuko ukiwemo Ebola

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea kituo cha kutibu magonjwa ya mlipuko na ambukizi cha Temeke (Temeke Isolation Center) pamoja na Kipawa ikiwa ni hatua ya kuona utayari wa vituo hivyo kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa Ebola iwapo utaripotiwa hapa nchini.
Mheshimiwa Waziri Ummy amefanya ukaguzi katika vituo hivyo vilivyopo jijini Dar es Salaam huku akisisitiza mafunzo zaidi kwa watumishi na vifaa kinga.

“Tuliweza kuishi na corona, ukisoma WHO watu 10 angalau vifo ni asilimia 40, kwa sababu ya maendeleo ya matibabu tunaweza kuokoa watanznaia wengi. Hakuna chanjo ya Ebola kirusi cha Sudan, ila kwa aina ya Zaire chanjo ipo, hili ni jambo kubwa na gumu tuendelee kuomba isiingie kwetu.

“Lakini Wizara tunazidi kujiimarisha akitokea mgonjwa tunampeleka wapi, tusianze kuhangaika. Nimefika hapa kukutana na Timu ya Haraka Mkoa wa Dar es Salaam (Rapid Response Team) kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.

"Virusi vya Ebola ni tishio kubwa zaidi, kwani mtu akiambukizwa hushambulia mwili wake ikiwemo viungo muhimu ndani ya mwili wake (ini na figo) na hatimaye kifo hasa ikiwa hatapata tiba yoyote ile.

"Mashambulizi hayo ya viungo ndani ya mwili ndiyo ambayo husababisha mtu kutoka damu sehemu mbalimbali za mwili wake. Si ugonjwa m-laini tuliweza kuishi na Corona, lakini si Ebola, Ebola inakulaza kitandani ni tishio,”amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

“Ebola ni tishio jana Waziri wa Afya wa Uganda ameniambia wamepata wagonjwa wapya watano inafanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko (Septemba, 2022) kufikia sasa ni jumla ya watu 126. Waliolazwa 54 na vifo 32 vimethibitika. Uganda kufikia sasa wanafuatilia watu 2,183 ambao walikuwa karibu na watu waliothibitishwa kuwa na ebola.

“Wasiwasi wetu unazidi baada ya kuwa ugonjwa umeingia Kampala na Entebbe kwa hiyo ndege zinazokuja kutoka Kampala, kuja Dar es Salaam na mabasi.Kuibuka kwa Ebola Uganda kunaiweka Tanzania katika hatari ya kupata mlipuko huu kutokana na mwingiliano mkubwa wa kiuchumi na kijamii na Uganda.

“Tunaiona hatari kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sababu ugonjwa tayari upo Kampala na Entebbe na hivyo Waziri wa Afya wa Uganda ameahidi kuipa Tanzania orodha ya wahisiwa wa Ebola ili wasiweze kuruhusiwa kabisa kuingia Tanzania,"amesema.

Pia amesema, Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo limeahidi kuleta nchini Tanzania wataalamu ambao waliwahi kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola ikiwamo huko Liberia na kusisitiza hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa Ebola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news