Rais Samia akemea tabia za udokozi wa vifaa katika miradi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.

Jiwe hilo ameliweka leo Oktoba 30, 2022 huku akiwataka Watanzania watakaopata fursa ya ajira katika mradi huo kuacha vitendo vya wizi wa vifaa kwenye mradi huo.

”Ndugu zangu najua kuna tabia za baadhi ya wale mnaopewa kazi za muda (vibarua) wakipewa kusimamia ujenzi wanakuwa na vijitabia vya kudokoa dokoa mara mfuko wa misumari,mara saruji, hii sio sawa nataka mtakaopata nafasi msijihusishe na vitendo hivo;
Hafla hiyo imefanyika katika Kata ya Msalato iliyopo jijini hapa ambapo mradi huo wa njia nne za ndege utatekelezwa kwa awamu mbili na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 600 hadi kukamilika kwake.

Mheshimiwa Rais amewataka wananchi wa Dodoma na wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha kazi zinazoweza kufanya na watanzania wapewe kipaumbele.

Amesema kuwa, ujenzi huo lengo ni kukuza ushindani unakuwepo wa kimataifa na pia ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani ndege za kimataifa zitakuwa zikiendesha safari zake na pia soko la bidhaa litaongezeka. 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa amesema, mradi huo utakuwa na fursa kwa wakazi wa Dodoma na mikoa mingine pamoja na kuiunganisha nchi na mataifa mengine na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo umalizike kwa wakati.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kumuunga mkono Rais Samia.

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila amesema kuwa eneo hilo lina ukubwa wa hekta 4500 na shilingi Bilioni 15.20 zimetumika kulipa fidia wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya mradi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news