Tanzania yang'ara uchanjaji chanjo ya UVIKO-19

NA MWANDISHI WETU

MRATIBU Kiongozi Kimataifa wa Ubia wa Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, Bw. Ted Chaiban ameipongeza Tanzania na nchini nyingine barani Afrika pamoja na wadau wa Sekta ya Afya kwa uhamasishaji na kuchanja wananchi chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Bw. Ted Chaiban amebainisha kuwa, Tanzaina imeshika nafasi ya pili kwa kiwango cha juu cha uchanjaji huku ikiwa imefikia asilimia 37.9 ya uchanjaji wananchi kwa mujibu wa takwimu za kidunia.

Katika kusisitiza hilo, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wadau wa maendeleo,watumishi wa afya na watu wengine waliowezesha kufanikisha jitihada hizo za kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Afrika kwa kiwango cha juu cha uchanjaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news