TANZIA: Prof.Emmanuel Kigadye wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) afariki

NA DIRAMAKINI

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof.Elifas Bisanda anasikitika kutangaza kifo cha Prof.Emmanuel Kigadye (pichani) kilichotokea Oktoba 29, 2022 katika Hospitali ya Bochi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 30, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dkt.Mohamed Maguo imefafanua kuwa,mpaka umauti unamkuta, Prof.Kigadye alikuwa ni Profesa Mshiriki katika Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Taaluma za Mazingira.

Prof.Kigadye amefanya kazi ya kufundisha, kutafiti, kushauri kitaalamu na huduma kwa jamii kwa muda mrefu na hivyo kutoa mchango wake kwa maendeleo ya nchi yetu.

Vilevile, Prof.Kigadye amehudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi na mpaka anafariki alikuwa ni Mkurugenzi wa Utafiti, Machapisho na Ubunifu wa OUT.

Post a Comment

0 Comments