TANZIA:Mwanahabari na Mkurugenzi gazeti la Tanganyika Tanzania afariki

NA MWANDISHI WETU

MWANDISHI wa habari mwandamizi,Bw.Frank Mbunda amefariki dunia Oktoba 16, 2022 katika Hospitali ya Mkoa General Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa juzi jioni.

Mtoto wa marehemu, Ashery Mbunda alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa taratibu za maziko zinafanyika Makole jijini Dodoma nyumbani kwa mlezi wake wa kiroho.

Mke wa marehemu, Yunice Mbunda amesema leo Oktoba 17 itafanyika misa ya kumuombea marehemu katika Kanisa la Anglikana Makole Dodoma na Oktoba 18, 2022 mwili wake utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ambako taratibu za maziko yake zitafanyika.

Marehemu Frank Mbunda ameacha mjane na watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

Frank Mbunda enzi za uhai wake amewahi kuandikia magazeti mbalimbali na hadi kifo chake alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kinarani Co.General Publishers and Printing iliyokuwa ikichapisha gazeti la Tanganyika Tanzania.

Post a Comment

0 Comments