TBA yataja sababu ya kufanya vizuri tasnia ya majengo

NA DIRAMAKINI

MENEJA wa Mawasiliano kwa Umma na Masoko wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Bw. Fredrick Kalinga amesema kuwa wanaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya majengo kwa sababu ya uzoefu wa zaidi ya miaka 20 na kuwa na wataalam na vifaa vya kutosha.
PICHA NA DIRAMAKINI.

Amesema hayo Oktoba 3 ,2022 katika viwanja vya EPZ katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini Kitaifa yanayoendelea Mjini Geita katika banda la wakala huo.

Amesema kuwa, TBA imeshiriki maonesho hayo ili kuwaonesha wananchi wa Geita na mikoa jirani miradi ambayo inaitekelezwa katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na majengo ya ofisi,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita majengo matatu.

Majengo matano katika Hospitali ya Kanda ya Chato,na majengo ofisi sita ambayo wamejenga maeneo mbalimbali ya mkoa ikiwemo ya Shirika la Umeme (TANESCO),mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya pamoja na Ofisi ya TBA.

Aidha, amesema kuwa TBA ina mradi mkubwa wa nyumba 3,500 za watumishi wa umma Mzuguni mkoani Dodoma ambazo zikikamilika zitatumika na watumishi wa umma.
PICHA NA DIRAMAKINI.

Ametaja miradi mingine kuwa ni pamoja na majengo ya wizara na taasisi 28 yaliyobuniwa na yanajengwa na TBA katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma.

Kalinga ameongeza kuwa, kwa sasa TBA haina malalamiko ya kuchelewesha miradi ya majengo kukamilika kwa sababu serikali ilitoa kibali cha ajira na kuajiri wafanyakazi na wataalam wa kutosha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news