Ufunguzi wa mkutano wa wadau wa demokrasia Zanzibar

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Othman Masoud Othman leo Oktoba 4, 2022 amejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, Siasa, dini na wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kushiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Kujadili Masuala Mahsusi ya Zanzibar yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa.


Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar, mbapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments