TRA yafunguka madai ya Mama Kibonge wa Kariakoo

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’ kwa Serikali kuwa ilikuwa inakusanya kodi kwa kutumia mabavu eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam muda wa saa saba usiku kwa mfanyabiashara aliyefahamika kama Mama Kibonge.

“Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa ufafanuzi kwa umma kuwa, zoezi lililokuwa likifanyika kwenye stoo za mfanyabiashara huyo eneo la Kariakoo ni ukamataji wa shehena za vitenge zilizoingizwa nchini kwa njia ya magendo.
"TRA imekuwa ikifuatilia tuhuma zilizokuwa zikitolewa dhidi ya mfanyabishara huyo za uingizaji wa bidhaa za vitenge nchini kwa njia za magendo ambapo hivi karibuni uchunguzi wetu ulibaini kuwa, kulikuwa na makasha mawili yenye mizigo ambayo nyaraka zake zilionesha kuwa bidhaa zilizokuwa ndani yake zilikuwa ni mashuka zikielekea Chitipa Mzuzu nchini Malawi.

“Hata hivyo, bidhaa hizo hazikuwa mashuka kama nyaraka zilivyoonesha bali zilikuwa ni vitenge vinavyotarajiwa kuingizwa nchini pasipo kulipiwa kodi (dumping) na zilihusishwa na Mfanyabiashara huyo, shehena hizo baada ya kutoka Bandari ya Dar es Salaam usiku saa 7 na dakika 56, kasha moja lililokuwa limepakiwa kwenye Lori namba T680 AGN / T439 AEB linalomilikiwa na Yusuph Suleiman lilipofika maeneo ya Tabata Matumbi, lilichepuka kuingia kwenye maghala ya bidhaa ambapo Kikosi chetu cha Kuzuia Magendo kwa kushirikiana na Polisi walikuta lori hilo limeanza kushusha shehena hiyo ambayo ilithibitika kuwa ni marobota 290 ya vitenge na sio mashuka kama nyaraka zilivyoonesha.

“TRA inawahakikishia Wafanyabiashara na watanzania wote kwa ujumla kuwa, itaendelea kukusanya kodi kwa weledi kama ilivyoelekezwa na Rais Samia, aidha, TRA inatoa onyo kwa Wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya ukwepaji kodi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news