WAZIRI BALOZI DKT.CHANA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA UVIKO-19

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuipatia Wizara ya Maliasili na Utalii kiasi cha Shilingi Bilioni 90.2 zilizotumika kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu ya utalii badala ya kuitumia fedha hiyo kununulia barakoa na vitakasa mikono pekee kama nchi nyingine za Kiafrika zilivyofanya.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa kwenye kikao cha kujadili matumizi ya kiasi cha Sh.Bilioni 90.2 ilizoidhinishiwa Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya sekta ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza Jijini Dodoma na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu matumizi ya kiasi cha Sh.Bilioni 90.2 ilizoidhinishiwa Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya sekta ya utalii.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 23, 2022 Jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu matumizi ya kiasi cha Sh.Bilioni 90.2 ilizoidhinishiwa Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya sekta ya utalii.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akizungumza Jijini Dodoma na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambapo amewaeleza kuwa fedha za UVIKO 19 zimesaidia kununua magari nane ikiwa ni vitendea kazi vya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kulia ni .Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana.

Amesema fedha hizo zimetumika kukarabati na kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege ndani ya hifadhi, ununuzi wa mitambo na magari, vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya shughuli za ulinzi na uhifadhi, ujenzi wa vituo vya taarifa, mageti ya kuingilia pamoja na kuimarisha shughuli za mafunzo na utafiti na hivyo kuifanya Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kutekeleza lengo la kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano (5) na mapato yatokanayo na Sekta ya Utalii kufikia Bilioni sita (6) ifikapo 2025.
Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakishiriki kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii cha kujadili matumizi ya kiasi cha Sh.Bilioni 90.2 ilizoidhinishiwa Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya sekta ya utalii.

''Fedha za UVIKO zimesaidia kuboresha miundombinu na kufungua barabara mpya ndani ya hifadhi zetu ambazo zimewezesha magari ya watalii kufika mahali ambako kulikuwa hakufikiki,'' amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.

Akizungumzia kuhusu matumizi ya fedha hizo kwa upande wa TANAPA, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amesema fedha hizo zimenufaisha jumla ya Hifadhi za Taifa 22 ambapo mitambo seti za mitambo iliyonunuliwa ikiwemo ile ya kutengeneza barabara imepelekwa katika kanda nne za Uhifadhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Consolata Kapinga akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii waliokuatana leo Jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Pindi Chana amesema fedha hizo za UVIKO zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Utalii ambapo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Makumbusho ya Taifa na Idara ya Utalii zimenufaika kwa kuboresha miundombinu ya utalii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Juma Ally Makoa (Mb) akizungumza mara baada ya wasilisho la utekekelezaji wa wa shughuli na miradi mbalimbali ya sekta ya utalii ambapo ameitaka Wizara kuikalisha miradi hiyo kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Juma Ally Makoa (Mb) amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikifanya vizuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kulinda,kuhifadhi na kuendeleza maliasili zilizopo nchini ili ziendelee kuwanufaisha Watanzania wote akitoa wito Wizara kusimamia miradi iliyobaki ili iweze kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia thamani ya fedha.

‘’Sisi ni kama Wajumbe wa Kamati hii ni mategemeo yetu kuona fedha hizi zinatatua changamoto ya miundombinu ili watalii wanaotembelea hifadhi zetu wafurahie utajiri tulionao,"amesema Mhe.Makoa.

Post a Comment

0 Comments