BODABODA MANYARA WAMPOKEA RAIS SAMIA KWA KISHINDO

NA DIRAMAKINI

UJIO wa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mkoani Manyara umepokelewa kwa kishindo na vijana wa boda boda ambao waliamua kufanya maandamano makubwa ya kumpokea Kiongozi huyo wa Kitaifa.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kumpokea Rais Samia kwa njia ya maandamano,vijana hao wa boda boda wamesema, sababu ya kumpokea kwa maandamano ni kutokana na sasa bodaboda kufanya kazi zao bila budugha, pamoja na kuhakikishiwa usalama wao kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Aidha, bodaboda hao pia wameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuwa mikopo ya asilimia nne, kupitia Halmashauri ya Babati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news