BREAKING NEWS:Ajali yajeruhi wafungwa, askari wilayani Kiteto

NA DIRAMAKINI

WAFUNGWA kadhaa wakiwemo askari magereza wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo Novemba 8, 2022 katika eneo la Kaloleni wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,Mbaraka Batenga amethibitisha tukio na kusema kuwa, chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. Jitihada zinaendelea kufanywa na askari wa usalama barabarani kujua chanzo cha ajali hiyo.
Amesema, gari hilo lilikuwa linatoka kambini kwenda katika shughuli za kila siku za kawaida.Taarifa zaidi zinakujia hapa DIRAMAKINI

Post a Comment

0 Comments