Dereva mzembe akamatwa baada ya kuwajeruhi mama na watoto wake wawili

NA DIRAMAKINI

KURUGENZI Kuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani (Muroor) mjini Madina, Saudi Arabia imemkamata dereva mzembe ambaye alimjeruhi mama mmoja na watoto wake wawili.

Askari wa usalama barabarani, bila kumtaja jina lake walifanikiwa kumkamata dereva huyo baada ya video fupi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiendesha gari lake kwa uzembe.

Uendeshaji huo wa kizembe ulisababisha gari lake kuyumba barabarani na kugongana na magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni.

Ajali hiyo ambayo ingesababisha kifo cha mama huyo na watoto wake wawili, ilisababisha watatu hao kupata majeraha madogo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Saudi Arabia, watatu hao walikuwa wametoka kwenye nyumba iliyokuwa karibu na walikuwa wakitembea karibu na magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa.

Watu wengi waliosambaza video ya dereva aliyeshindwa kulidhibiti gari lake walitaka aadhibiwe mara moja. Ajali hiyo ilitokea katika Kitongoji cha Al-Hamra mjini Madinah.

Polisi wamethibitisha kuwa, dereva huyo mzembe alifikishwa katika Mamlaka ya Trafiki ili kutumikia adhabu zilizowekwa kwa madereva wazembe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news