FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI ILI USINYANYASWE

NA MWAWAKILI WETU

LICHA ya kuwepo Jeshi la Polisi kupitia askari ambao wamepewa jukumu kubwa la kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao, kutunza sheria na utulivu miongoni mwetu ndani ya jamii tumekuwa tukiingilia majukumu hayo kwa kujipa mamlaka ambayo hatujapewa.
Hii inamaanisha kuwa, kuibuka kwa makanjanja ambao wanajifanya kuwa askari miongoni mwa jamii huku wakiwa hawana vigezo hivyo, wamekuwa wakiisababishia maumivu jamii na hata kuchangia dhuluma mbalimbali katika jamii.

Ili kuepuka hayo, jopo la mawakili limekaa chini na kuainisha mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyafahamu ili usifanyiwe dhuluma na makanjanja hao au kufanyiwa manyanyaso uwapo mikononi mwa polisi. Miongoni mwa mambo hayo ni;

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwe nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.


Kumbuka Jeshi la Polisi lina Jukumu la Kulinda Usalama wa Raia na Mali zao

Jukumu kubwa la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao kwa kutunza amani na usalama, kutunza sheria na utulivu, kuzuia na kutambua uhalifu, kukamata na kutunza wahalifu na kulinda mali. Idara za Jeshi la Polisi ni pamoja na:

 1:Divisheni ya Operesheni;

2:Divesheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai;

3:Devisheni ya Intelijensia. 

4:Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu. 

Jeshi la Polisi linaongozwa na Inspekta Jenerali wa Polisi akisaidiwa na Naibu Kamishna Jenerali wa Polisi wakisaidiwa na Makamishna wa Divisheni, Kanda, Vitengo, Makamanda wa Vikosi mbalimbli na wa Mikoa, Wilaya na Vituo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news