Japan yawaonjesha Ujerumani kichapo cha kushangaza Qatar

NA DIRAMAKINI

UJERUMANI imeonja kichapo cha kushangaza cha mabao 2-1 dhidi ya Japan katika mechi ya ufunguzi ya Kundi E ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Picha na Reuters.

Ni kupitia mtanange ambao umepigwa Novemba 23, 2022 ambapo mshambulizi wa Kijapani Daizen Maeda alifunga bao la mapema dakika ya nane, lakini halikuruhusiwa kwa sababu ya kuotea kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa, Al Rayyan nchini Qatar.

Baadaye kipindi cha kwanza, Ujerumani walipata penalti dakika ya 32 iliyotumbukizwa nyavuni dakika ya 33 na mchezaji wa kulipwa wa Ujerumani ambaye ni kiungo wa Manchester City, ilkay Gündoğan baada ya beki David Raum kuangushwa na kipa Shuichi Gonda.

Pia Kai Havertz alifunga bao katika dakika ya 45, lakini lilikataliwa baada ya ukaguzi wa Refa msaidizi wa video (Video assistant referee-VAR) kufanyika.

Japan walisawazisha wakati Ritsu Doan alipomaliza kiu yake kwa kutupia shuti kali dakika ya 75. Aidha, timu ya taifa ya Japan ilikoleza moto wake ambapo Takuma Asano ndani ya dakika ya 83 aliwanyanyua mashabiki wa Japan tena.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news