Kocha Nabi awabwaga Mubiru na Hitimana katika tuzo za TFF

NA DIRAMAKINI

KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Oktoba katika msimu wa mwaka 2022/23.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana jijini Dar es Salaam siku ya Novemba 12, 2022 kilimchagua Nabi.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kocha Nabi aliwashinda Mubiru Abdallah wa Mbeya City na Thiery Hitimana wa KMC alioingia nao fainali, ambapo mwezi huo Yanga SC iliifunga Ruvu Shooting mabao 1-2.

Pia iliifunga KMC bao 1-0 na Geita Gold pia bao 0-1, huku ikitoka sare na Simba SC ya jijini Dar es Salaam kwa bao moja.

Wakati huo huo, Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Sokoine uliopo mkoani Mbeya, Modestus Mwaluka kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Septemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Post a Comment

0 Comments