Sixtus Sabilo wa Mbeya City ndiye shujaa wa Oktoba

NA DIRAMAKINI

SIXTUS Sabilo wa timu ya soka ya Mbeya City amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2022/23.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana jijini Dar es Salaam siku ya Novemba 12, 2022 kilimchagua Sabila baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Oktoba na kutoa mchango mkubwa kwa Mbeya City.

Sambamba na kufunga mabao mawili na kuhusika na mengine matatu katika michezo minne ambayo Mbeya City ilicheza.

Mbeya City ilifunga Polisi Tanzania mabao 3-1, pia iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0 na kutoka sare ya mabao 2-2 na mtibwa Sugar huku ikitoka sare ya bao moja na Ihefu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sabilo aliwashinda beki Dickson Job wa Yanga na kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza wa Geita Gold pia bao 0-1 huku ikitoka sare na Simba SC ya bao moja.

Post a Comment

0 Comments