Lionel Messi: Tumekufa, ni pigo gumu sana

NA DIRAMAKINI

“Tumekufa. Ni pigo gumu sana,” Haya yalikuwa majibu ya Lionel Messi aliyeonekana kuchanganyikiwa baada ya kushindwa na Saudi Arabia katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia.
Hakuweza kuzuia hisia zake baada ya kudundwa.(Picha na Getty Images).

Ni baada ya timu yake ya Taifa ya Argentina kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Saudi Arabia kupitia michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

Mtanage huo umepigwa Novemba 22, 2022 katika dimba la Lusail Iconic Stadium (Lusail Stadium) lililopo mjini Lusail, Qatar.

Kupitia kundi hilo la C, Messi alikiri Argentina haiwezi kuwa na visingizio vya kushindwa. Licha ya kupata bao la kwanza katika kipindi cha kwanza ndani ya dakika ya 10 kupitia mkwaju wa penalti ambao ulitupiwa kambani na Messi mwenyewe. 
 
Saudi Arabia walionesha utulivu, kwani dakika 45 za kwanza zilitamatika kwa Argentina wakiwa na bao kibindoni. Kipindi cha pili kilianza kwa ambapo dakika ya 48 Saleh Alshehri alisawazisha bao hilo.

Kabla Argentina awajapoa kupitia michuano hiyo yenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani, Salem Aldawsari wa Saudi Arabia aliwanyanyua mashabiki wa taifa lake kwa kutupia bao tamu nyavuni ndani ya dakika 53

Baada ya mchezo huo, Messi hakuweza kuficha hisia zake ambapo alionekana wazi kukata tamaa. “Hatukutaka kuanza hivyo. Tulitaka kushinda, kuipa akili amani. Hakuna visingizio. Sasa, ni wakati wa kuzingatia nguvu na umoja wa kikosi. Ni wakati wa sisi kuwa na umoja zaidi kuliko hapo awali. Ni wakati wa kutulia.”

"Ni kipigo kigumu, kipigo kichungu. Tunapaswa kuendelea kujiamini. Hebu tujaribu kuishinda Mexico ili kuona jinsi kundi litakavyokuwa." Akitathmini mchezo huo, Messi alikiri Argentina walitoka nje kwa kasi sana na hawakuweza kuendelea.

"Tulikuwa na nafasi na tulipata nafasi nyingi za kuotea," alisema. "Tulifanya makosa ya kuongeza kasi sana. Tulijua watacheza na safu ya juu. Tuliongeza kasi kidogo, lakini baada ya hapo, tulianza kuchanganyikiwa, kupoteza uchezaji na kupoteza pambano.”

“Bao la mapema kipindi cha pili lilituchanganya. Hatukuweza kupata mchezo ambao tumekuwa tukionyesha kwa muda mrefu. Mchezo ulipoendelea, matokeo dhidi yetu yalizidi kuwa magumu,” aliongeza.

Post a Comment

0 Comments