NA MWANDISHI WETU
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Dkt.Hashil Abdallah amezishauri taasisi za umma pamoja na watendaji wake wanaotoa huduma kuhakikisha wanaweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji ili kifikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita na kuliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kati wa Juu.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi, Mhe. Salma Maghimbi amesema Baraza hilo litaendelea kutenda haki katika maamuzi yake kwa kuzingatia sheria, kanuni taratibu pamoja na ushahidi na udhibiti unaotolewa kwa lengo la kuendeleza biashara, kuvutia uwekezaji na hatimae kukuza uchumi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Bw. William Erio amesema FCC inashirikiana na FCT katika kuliwezesha Baraza kufanya maamuzi ya kesi zinazowasilishwa kwa Baraza hilo kutoka Mamlaka za Udhibiti mbalimbali ili kuhakikisha biashara zinaendelea kwa kizingatia usawa katika ushindani wa soko.

Aidha, amesema Baraza hilo limepewa hadhi ya Kimahakama ya utoaji haki kwenye masuala ya Ushindani Udhibiti wa Soko naKumlinda mlaji. Maamuzi ya kesi za rufaa na maombi yanayotolewa na Baraza hilo ni ya mwisho.