MIFUKO 400 YA MBOLEA YA RUZUKU YAKAMATWA IKITOROSHWA NCHINI

NA MWANDISHI WETU

KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe imefanikiwa kukamata shehena ya mbolea mifuko 403 katika Kijiji cha Chitete kata ya Chitete ikivushwa kwenda nchi jirani ya Malawi.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amesema, gari mbili zilizobeba zaidi ya mifuko 400 ya Mbolea ya Ruzuku zimekamatwa wilayani Ileje mkoani Songwe katika Mpaka wa Tanzania na Malawi zikivusha mbolea hizo kwa njia za zisizo rasmi pamoja na pikipiki moja ambayo ilitumika kwa ajili ya kuongoza njia ya magari hayo

DC Gidarya amesema walipokea taarifa kutoka kwa mwananachi mmoja kuwepo kwa tukio hilo ambapo hadi wanafika katika eneo la tukio tayari gari moja ilikuwa imeshavusha mbolea hizo na kutokomea kusikojulikana hivyo kufanikiwa kukamata gari namba T. 463 CNN ilibeba mifuko 201 na gari namba T. 202 DGU ilibeba mifuko 202.

Katika hatua nyingine Gidarya ametoa onyo kwa viongozi ambao watatajwa kuhusika na mchezo huo mchafu wa kuihujumu serikali kwamba watachukiliwa hatua kali za kisheria.

"Nitamke tu mtu yeyote atakaebainika amehusika na huu mchezo wakati Mheshimiwa Rais anapamabana hatutamuacha salama maana atakuwa anatukwamisha kimaendeleo," amesema Gidarya.
Pia Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa, bei ya mbolea ya Tanzania ipo chini kutokana na uthubutu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

"Mbolea hii imekamatwa ikisafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi ambako wenzetu wanauza mfuko mmoja laki moja na elfu kumi (110,000),hivyo tutahakikisha tunawakamata wanaovusha mbolea serikali imewekeza bilioni 150 kupunguza makali kwa wakulima," amesema Gidarya.
Aidha, Gidarya amewataka wananchi na viongozi kuendelea kutoa ushirikiano pindi vitendo kama hivyo vinapotokea.

Post a Comment

0 Comments