MSIWASIKILIZE WAKOMBOZI WA UONGO

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wa Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma wameambiwa kuwa kabla ya mwisho wa Dunia yatatokea mengi ya kutisha, mengi hayo yatakuwa ni ya ulaghai, ya ushawishi wa kumuacha Mungu na kuwasikiliza wakombozi wa uongo, hivyo kila mmoja anapaswa kumuomba Mungu amsadie kutonaswa na hila hizo.
Hayo yamesemwa kanisani hapo katika maombi ya Jumapili ya 33 ya mwaka C katika misa ya kwanza iliyosalishwa na Padri Paulo Mapalala wakati wa utangulizi wa maombi ya domnika hiyo.

Utangulzi huo ulifuatiwa na maombi matano huku majawapo ya maombi hayo ni hili, “Utupe moyo wa kutokubali kushindwa kwa ubaya, bali tushindane ubaya kwa wema.”

Maombi hayo yalihitimshwa na Padri Mapalala akisema, “Ee Mungu wa Milele, ulitujalie imani ituimarishe katika misukosuko ya dunia, uyasikilize maombi yetu na utuongoze tushike kwa uthabiti maneno ya mwanao Yesu Kristo.”

Awali katika mabubiri ya misa hiyo yaliyokuwa mafupi mno ya dominika za mwisho mwisho za mwaka C, mwaka wa liturujia ya kanisa, Padri Mapalala alitisitiza,

“Ulimwengu wa leo umejaa mambo mengi, fujo nyingi, vituko vingi, magomvi mengi na vita vile vile lakini Kristo anatutuliza na kutuambia kuwa mambo hayo hayana budi kuja. Vurumai na vurugu katika familia, vurugu katika jumuiya, vurugu katika jamii zitakuwepo, pengine kusingiziana, kusemana mabaya lakini jipeni moyo, kama mtafanya kwa ajili ya jina lake Mungu, yeye atatufundisha vya kujibu.”

Wakati wakristo hao wakisali misa hii hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu bado ni ya jua kali huku sasa kukiwa na dalili na jua kupungua kwa vipindi fulani vifupi vifupi huku wakazi wa eneo hilo wakiamini kuwa mwaka huu mvua zitaanza kunyesha mapema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news