Mtaalam na Mbobezi wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali, Yusuph Kileo awauma sikio Watanzania kuhusu 'Mobile Apps'

NA DIRAMAKINI

MTANZANIA ambaye ni Mtaalam na Mbobezi wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali, Yusuph Kileo ameendelea kutoa wito kwa watumiaji wa simu janja kuongeza umakini ili kuepuka kulipa gharama.

"Natoa wito kwa watumiaji wa simu janja kuongeza umakini kwenye Mobile Apps wanazo install kwenye simu;
Kileo amekuwa mstari wa mbele kutoa angalizo na tahadhari mbalimbali zinazohusiana na uhalifu wa mitandaoni ambapo hivi karibuni alieleza pia namna ambavyo uhalifu wa mtandao aina ya Social Engineering (S.E) Attack unavyoanza kushika kasi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema, wahalifu wengi kwa sasa wanatumia uhalifu wa S.E attack hususani nchini Kenya kwa kuwasiliana na watu ambao huwaaminisha kuwa,wao ni wahudumu wa benki halisi, hivyo mwisho wa siku mhanga wa uhalifu huo anajikuta amewapatia taarifa zake zote, jambo ambalo ni hatari.

S.E attack ni aina ya uhalifu ambao umekuwa maarufu zaidi mtandaoni ambapo wahalifu huwa wanawateka wananchi au wateja wa benki kisaikolojia kwa kuwahadaa ili kutoa taarifa nyeti zinazowahusu.

Kupitia aina hii ya uhalifu, mhalifu kwanza huchunguza mwathiriwa anayekusudiwa ili kuweza kukusanya taarifa muhimu zinazomuhusu, mashambulio ambayo kwa sasa nchini Kenya inatajwa kuwa, kati ya matukio 1000 ya kupigiwa simu,mpokeaji simu mmoja ujikuta akiwapa taarifa zote wahalifu hao na kujipatia fedha zake.

"Kikubwa zaidi, nashauri elimu zaidi indelee kutolewa kwa watu wetu hasa ukizingatia kuna changamoto za watu wengi kutoelewa namna ya kubaki salama watumiapo mitandao na kufanya miamala mtandao.

"Uhalifu mtandao unakuja na mbinu mpya na hili la mhanga (victim) kupokea simu kama imetoka kwa benki halisi au mtandao wa simu limeanza kushika tena kasi.

"Mara kadhaa nimekua nikisema uhalifu unaofanyika sehemu moja unaweza kufanyika sehemu nyingine pia, hivyo tuendelee kuchukua tahadhari ili kubaki salama,"amefafanua Kileo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news