Rais Dkt.Mwinyi akaribisha wawekezaji kutoka Somalia

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Balozi wa Shirikisho la Somalia nchini Tanzania,Zahra Ali Hassan.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Novemba 23, 2022 Ikulu jijini Zanzibar baada ya Balozi Hassan kufika kwa ajili ya kujitambulisha.

Dkt.Mwinyi amewaomba wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Somalia kuja Zanzibar kwa ajili ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo uanzishaji wa nyumba za makazi.

Alisema Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji, huku akibainisha miradi ya uanzishaji wa nyumba za makazi kuwa ni eneo lenye fursa pana kwa ajili ya kuwekeza.

Aidha, amepongeza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Somalia na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, ambapo wananchi wa nchi hizo wamekuwa na maingiliano ya muda mrefu pamoja na kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kijamii pamoja na kibiashara.

Naye Balozi wa Shirikisho la Somalia nchi Tanzania, Zahra Ali Hassan alishukuru ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wananchi wa nchi mbili hizo, huku akibainisha azma ya wananchi wa Somalia kuendeleza ushirikiano huo kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali pamoja na kuimarisha biashara.

Post a Comment

0 Comments