Rais Samia aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika katika ukumbi wa Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 12,2022.(Picha na Ikulu).
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ukumbi wa Chamwino Dodoma akihudhuria Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla.

Post a Comment

0 Comments