Rais Samia aongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dodoma

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto), Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango na (kulia) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe.Dkt Tulia Akcson, wakiwa katika ukumbi wa White House Dodoma, wakihudhuria Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo Novemba 13, 2022 na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu).
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo Novemba 13, 2022.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) wakiwa katika ukumbi wa White House jijini Dodoma wakihudhuria Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa , kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika ukumbi huo leo Novemba 13, 2022.(Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments