Rais Samia Kutunukiwa Tuzo ya Kiongozi wa Kimageuzi Afrika (Transformation Leadership Award) leo

NA MWANDISHI MAALUM

WAANDAAJI wa tuzo hizo za muziki zinazotolewa na dispora wa Afrika walioko nchini Marekani katika mawanda ya sanaa mara chache sana mbali ya kategoria za kawaida za muziki pia hutoa tuzo maalum kwa kiongozi wa kisiasa anayeleta mageuzi hasa katika sanaa barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ya viongozi wa Afrimma iliyotolewa Dallas, Texas, Marekani leo, jopo la wachambuzi wao wameona kuwa kitendo cha Rais Samia kurejesha tuzo kwa wasanii zilizokuwa zimekufa kwa miaka mingi na kushiriki Filamu ya Royal Tour, ni miongoni mwa sababu zilizompa alama nyingi Rais Samia miongoni mwa viongozi wengine wa Afrika kwa mwaka huu.
Rais Samia anakuwa Rais wa Tatu Afrika na Kiongozi wa Juu wa Kwanza Mwanamke Afeika kushinda Tuzo hiyo baada ya mwaka 2015 tuzo hiyo kwenda kwa aliyekuwa Rais wa Botswana LT. Gen. Dr. Seretse Khama Ian Khama na mwaka 2017 Tuzo hiyo kushinda aliyekuwa Rais wa Nigeria Chifu Olusegun Obasanjo.

Rais Samia anatarajiwa kukabidhiwa Tuzo hiyo usiku wa leo jijini Dallas wakati wa usiku wa Tuzo za Kimataifa za Afrimma sawa na Alfajiri ya Jumapili Novemba 20 kwa saa za Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news