RAIS SAMIA SULUHU AWEKA REKODI YA KIPEKEE DUNIANI

NA ABDULAZACK ABDUL

WACHAMBUZI wa siasa za Kimataifa na masuala ya uchumi wanaendelea kuhoji upekee wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kutokana na heshima kubwa aliyopewa na Rais wa China, Xi Jinping.
Mataifa mbalimbali yanaitazama Afrika kwa upekee, hivyo Rais Samia kukaribishwa nchini China kama kiongozi wa kwanza Afrika na kiongozi wa pili Duniani baada ya Rais Xi kuanza muhula mpya ni jambo kubwa linalothibitisha maendeleo.

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Baadhi ya mageuzi ni katika;

1. SERA YA MAMBO YA NJE:-Rais Samia amefanikiwa kurudisha heshima ya Tanzania kimataifa kwa kudumisha mashirikiano yenye tija na kushiriki kikamilifu katika agenda za kimataifa zenye faida si tu kwa Tanzania bali kwa Afrika na Dunia kwa ujumla. 

2. UWAZI NA UWAJIBIKAJI:-Rais Samia amefanikiwa kuzipa taasisi serikali na mashirika ya umma uhuru wa kuwajibika na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria ili kuongeza ufanisi. Hii imewezesha kutolewa ajira, kulipa malimbikizo, madeni, kupandisha watumishi madaraja na nyinginezo bila urasimu. 

3. UTAWALA WA SHERIA:-Rais Samia amefanikiwa kuupa muhimili wa Mahakama uhuru wa kufuata sheria katika utoaji haki na kuondoa kesi za kisiasa kwenye mahakama ili kudumisha misingi ya utawala wa sheria na utoaji haki. 

4. KUBORESHA HUDUMA KIJAMII:-Rais Samia anaendelea kufanikiwa kwa viwango vya juu katika kuboresha huduma za jamii. Mpaka sasa elimu inatolewa bure kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha Sita na Mikopo ya Elimu ya juu kwa wote wenye sifa.

5. KUSIKILIZA MAONI NA USHAURI:-Rais Samia amefanikiwa kutengeneza mazingira huru kwa wananchi kutoa mrejesho juu ya mambo mbalimbali na kutoa ushauri katika mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yao. Sifa hii ni ya kipekee sana kwa viongozi. 

6. UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI:-Rais Samia amefanikiwa kusimamia miradi kwa kufuata taratibu zinazoweza kutoa matokeo chanya badala ya mbwembwe zisizo na tija. Sifa hii ndio msingi wa mafanikio katika miradi mingi ambayo inampa faraja kila mtanzania mwenye akili timamu.

7. MAZINGIRA RAFIKI YA BIASHARA NA UWEKEZAJI:-Rais Samia amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa urasimu uliokuwa unakwamisha eneo hili muhimu ikiwa ni kwa kuondoa sheria zisizo na tija. Hii imepelekea kukua biashara katika sekta kama Utalii, Madini, Usafirishaji, Nishati, Kilimo, n.k.

Mambo haya na mengine mengi ya kihistoria ndio yanayovutia wawekezaji wengi na kuleta ustawi kwa wananchi. China ni kati ya wadau muhimu kwenye miradi ya Chuma, viwanda, bidhaa za kilimo, Vifaa na Teknolojia za TEHAMA n.k.

Kwa kipekee nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya, ndio hiyo inampa heshima kwa viongozi mashuhuri Duniani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news