Rais Samia:Wanasiasa msiwe kichocheo cha migogoro ya ardhi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wanasiasa kuacha kuwa kichocheo cha migogoro ya ardhi kwa maslahi yao binafsi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakati akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Catherine Magali aliyekuwa akielezea maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo Babati mkoani humo Novemba 23, 2022.

Rais Samia amesema hayo Novemba 23, 2022 wakati akihutubia wananchi wa Manyara kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kwaraa.

Aidha, Rais Samia amesema wanasiasa wamekuwa na tabia ya kutokuwachukulia hatua wananchi wanaovamia maeneo ya wenzao na badala yake huwatetea na kuwaunga mkono wavamizi hao kwa lengo la kupata kura baadae.

Rais Samia amesema tabia hiyo ya viongozi na wanasiasa inaharibu mipango ya matumizi bora ya ardhi, malengo ya Serikali na kuchelewesha kufikia maendeleo yaliyokusudiwa.

Rais Samia amewataka wanasiasa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kusimamia matumizi bora ya ardhi kwa kila mwananchi na kuwakemea wananchi wanaovamia maeneo ya ardhi ambayo hayakupangwa kwa matumizi hayo.

Rais Samia amekemea tabia ya wakulima na wafugaji kujichukulia sheria mikononi kwa kuwa kitendo hicho kinahatarisha amani na usalama wa nchi.

Awali, Rais Samia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Manyara ambayo ilianza kujengwa mwezi Novemba, 2018.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news