RATIBA YA MAZIKO YA ALIYEKUWA AFISA ELIMU SEKONDARI HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU MWALIMU EMMY MFURU

NA DIRAMAKINI 

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha unaendelea kutoa pole kwa Ndugu,Jamaa na Familia ya mpendwa wetu Mwalimu Emmy Mfuru ambaye alifariki tarehe 23 Novemba 2022 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.
Siku ya Jumatatu ya tarehe 28 Novemba 2022 itakuwa ni siku ya kumpunzisha mwenzetu kwenye nyumba yake ya milele ambapo ibada ya kuaga mwili itafanyika katika makazi ya marehemu Leganga kwa juu barabara ya pili baada ya kwa Mzunguu, taratibu hizo zitaanza saa 1:00 asubuhi.

Baada ya ibada ya kuaga mwili na salamu toka makundi mbalimbali, mwili utasafirishwa kwenda Moshi mjini kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme ambapo ibada ya maziko itaanza saa 9:00 alasiri .

BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE, AMEN

Post a Comment

0 Comments