Sasa ni Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mheshimiwa Rais Samia ametunukiwa shahada hiyo leo Novemba 30, 2022 wakati wa Mahafali ya 52 Duru ya Tano ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amemtunuku Mheshimiwa Rais Samia shahada hiyo katika mahafali yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City.

“Kwa mamlaka niliyokabidhiwa, ninakutunuku Digirii ya heshima ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hongera sana,”amesema Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati akimtunuku Rais Samia udaktari huo wa heshima kupitia mahafali hayo.

Ni baada ya maazimio ya Seneti ya Baraza la Chuo hicho katika kikako cha 876 kumpendekeza Rais Samia kutunukiwa shahada ya juu ya heshima ya falsafa kwa kile walichoeleza kuwa uongozi wake umeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini.

Sambamba na kuboresha elimu ikiwemo kujenga vyuo 25, kusaini na Benki ya Dunia mradi wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa lengo la kuboresha elimu ya juu nchini.

Mahojiano hayo yaliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati anaadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo alibainisha mengi ikiwemo safari yake ya elimu.
 
Mheshimiwa Rais Samia baada ya hatua hiyo, amemshukuru Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Baraza la Seneti la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kumpendekeza kupata tuzo hiyo na aliikubali kwa sababu siyo ya kwake pekee bali ni ya Watanzania wote.

"Suala la kupewa tuzo hii nimelipokea kwa unyenyekevu mkubwa. Lakini nilijiuliza maswali kadhaa sababu huko nyuma nilijaribu kuitafuta shahada hii, lakini muda haukunipa nafasi," amesema Rais Samia

Heshima hiyo kwa Mheshimiwa Rais Samia inakuja ikiwa ni miezi michache imepita wakati wa mahojiano maalumu yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kubainisha kuwa, alijaribu kufanya Shahada ya Uzamivu, lakini kutokana na majukumu mengi alishindwa huku akisema ataimalizia baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news