Picha tano, ajali ya Prado ilivyoua mama na watoto wake wakitokea katika mahafali

NA DIRAMAKINI

PICHANI ni muonekana wa gari namba T 597 BWU aina ya Toyota Prado likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali ikiwa imebeba familia ambayo ilitokea katika mahafali ya mtoto wao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Shule ya Sekondari Gili iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Katika ajali hiyo watu watatu ambao ni wanafamilia moja akiwemo mama na watoto wawili walifariki dunia na mmoja ambaye ni dereva Albert Mrema kulazwa katika chumba cha uangalizi maalum Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mlongazila).
Prado hiyo iliacha njia na kuingia bondeni mwishoni mwa wiki katika eneo la Kibamba Hospitali mkoani Pwani.
Waliofariki walitajwa kuwa ni Immaculata Byemerwa ambaye ni mama na watoto wake Janeth Byemerwa aliyekuwa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Marehemu Janeth alikuwa anasomea Uhandisi wa Ujenzi chuoni hapo huku Jollister Byemerwa ambaye ndugu zake walifika kusherehekea mahafali yake akiwa amehitimu kidato cha nne.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news