SUMAJKT yaunga mkono Kampeni ya Samia Nivishe Viatu

NA DIRAMAKINI

KATIKA kuunga mkono jitihada za Kampeni ya Samia Nivishe Viatu, Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) limeikabidhi Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao jozi 500 za viatu kwa ajili ya kuwavisha wanafunzi wa shule za msingi waishio vijijini.
Akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi jozi hizo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Muendeshaji wa kiwanda cha viatu vya ngozi na uzalishaji mali wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Mathias Peter John amesema SUMAJKT imeamua kuunga mkono kampeni hiyo ya kizalendo ya kusaidia wanafunzi.

Meja John amesema, lengo ni kurejesha tabasamu la watoto waishio vijijini hasa wanafunzi."Ni wakati wakati wakuweka tabasamu letu kwa wanafunzi hawa ili na wao wajisikie furaha, na watanzania wengine ungeni mkono jitihada za wenzetu na dhamira zao za kuwavisha viatu watoto walioko vijijini," amesema.

Pia amesema kiwanda hicho kimekuwa kikizalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu kwa ajili ya taasisi za ulinzi, viatu vya usalama( Safety boots), viatu vya maofisini na viatu vya watoto wa shule.
"Uwezo wa kiwanda hiki ni kuzalisha jozi 500 kwa siku kupitia Uzalishaji wa bidhaa hizi tumeweza kuandaa viatu kwa ajili ya watoto wa kutanzania walio shule za msingi.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanano, Steven Mengele amesema wamekuwa wakizunguka nchi nzima kuhakikisha watoto wasiovaa viatu wanaavaa.

Amesema kampeni hiyo ambayo ilianzia Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani na Tabora tayari wameshazifikia shule mbalimbali na kugwa jozi zaidi ya 500.

"Tumefika huko vijini unakuta mtoto anaanza darasa la kwanza hadi anamaliza la saba hajawahi kuvaa kiatu, hili nalo linachangia kushindwa kufaulu," amesema Mengele.

Aidha alitoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono kampeni hiyo ili watoto waishio vijijini nao waweze kuvaa viatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news