Tamasha la Kimataifa la Bagamoyo laja na maonesho maalum ya sanaa

NA JOHN MAPEPELE

KATIBU Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi ameongoza kikao cha Kamati ya kitaifa ya kuandaa Tamasha la Kimataifa la Bagamoyo ambapo amesisitiza kutakuwa na maonesho ya sanaa.
Dkt. Abbasi amesema haya Novemba 5, 2022 mjini Bagamoyo, kwenye kikao kazi cha maandalizi ya tamasha hilo la kihistoria.
"Ikiwa imebaki siku tano kuanza Tamasha la Kimataifa hilo, tayari maandalizi yote muhimu yamekamilika," amefafanua Dkt. Abbasi.

Amesema, tamasha la sasa limeshehena vionjo mbalimbali za Sanaa ikiwa ni pamoja na ngoma, sarakasi na komedi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Mbali na tamasha hilo kutakuwa na maonesho maalum ya Sanaa za Tanzania ili kutangaza Sanaa za Tanzania duniani.

Post a Comment

0 Comments