Rais Samia atoa pole ajali ndege ya Precision Air

NA DIRAMAKINI 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatilia ajali ya ndege ya Kampuni la Ndege ya Precision Air kuanguka katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo na kuongeza kuwa, "Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii".

Aidha, amewataka watanzania kuwa watulivu wakati zoezi la uokoaji likiendelea.

"Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie," amesema Rais Samia.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Novemba 6, 2022 na kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea kufanywa na Zimamoto, JWTZ pamoja na wavuvi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news