Tanzania imefanikiwa kulinda amani yake,UNHCR yawaeleza wahariri nchini

NA DIRAMAKINI

AFISA Muhifadhi Wakimbizi Mwandamizi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Tanzania, Boniface Kinyanjui amesema, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kulinda amani yake.
Kinyanjui alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye warsha ya siku tatu na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2022.

‘‘Amani haitoki juu kushuka chini, inalindwa na serikali, Serikali ya Tanzania imefanikiwa katika hili.…, Tanzania ni nchi ya amani lakini imezingirwa (na nchi zenye wasiwasi wa amani),’’ alisema.

Ofisa huyo alisema, Tanzania ni nchi iliyohifadhi wakimbizi kwa muda mrefu tangu uhuru na kwamba, ni miongini mwa nchi chache mabazo ziliruhusu baadhi ya wakimbizi kuwa raia wake.

‘‘Tanzania imepokea wakimbizi kutoka Ulaya, Marekani n ahata Kenya hapo. Ni miongoni mwa nchi chache zilizowapa wakimbizi uraia wan chi yake,’’ alisema.
Hata hivyo alisema, UNHCR hupenda zaidi zaidi kuona walimbizi wakipewa hifadhi pamoja na ruhusa ya kuendelea na maisha yao ya uzalishaji mali na si kuwekwa pamoja kwenye makambi.

‘‘Wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi sio watu wanaopendwa sana katika nchi nyingi. Sisi tungependa kuona wakimbizi wakipewa nafasi ya kujimudu kimaisha katika uzalishaji mali maana ni wanadamu kama wengine.

‘‘Katika wakimbizi kuna wataalamu wengi ambao wanaweza kusaidia jamii. Mfano; kuna mkimbizi alitoka Sudani Kusini na lipita Tanzania akaenda Afrika Kusini. Huko yeye ndiye aliyetengeneza mfumo wa kutoa maji kwenye mwili kupitia tundu za pua wakati ule wa UVIKO-19,’’ alisema.
Akizungumzia shirika hilo, Kinyanjui aliema UNHCR ilianzishwa mwaka 1950 na kwamba, mwaka 1951 ndio ilianza kuingia mikataba ya amani

‘‘Lengo kubwa la UNHCR ni kulinda haki ya mfungwa na mahitaji yake kokote atakapokuwa,’’ alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news