Uholanzi yaizima Senegal dakika za lala salama 2-0

NA DIRAMAKINI

CODY Gakpo na Davy Klaassen wa timu ya Taifa ya Uholanzi wamepeleka maumivu kwa timu ya Taifa ya Senegal baada ya kuachia risasi mbili za moto.

Davy Klaassen wa Uholanzi akishangilia baada ya kufunga bao la pili. (Picha na REUTERS/Dylan Martinez).

Ni risasi za mabao ambazo zimechomoka kwa kasi katika dimba la Al Thumama lililopo mjini Al Thumama nchini Qatar katika mtanange ambao umepigwa leo Novemba 21, 2022 ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022.

Licha ya Senegal kuonesha ukomavu ambao walikwenda dakika za mwanzo ubao ukisoma sufuri kwa sufuri, dakika ya 84 ya kipindi cha pili Cody Gakpo alifunga bao la dakika za lala salama katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia naye Davy Klaassen akaongeza la pili dakika 99 za lala salama na kuipa Uholanzi ushindi wa 2-0 dhidi ya Senegal katika mpambano wao wa Kundi A.

Kocha Louis Van Gaal alimkabidhi mlinda mlango Andries Noppert mechi yake ya kwanza ya kimataifa na hakuwa na la kufanya kwani safu ya ulinzi ya Uholanzi ilionekana kuwakandamiza mabingwa hao wa Afrika, ingawa aliokoa mkwaju mzuri dakika ya 73 na kuachia shuti kali la Idrissa Gueye.

Shambulizi la Uholanzi lilikuwa la kupoteza muda wote hadi Gakpo mwenye umri wa miaka 23 alipopenya katikati na kumshinda Edouard Mendy kwa mpira wa krosi kutoka kwa Frenkie de Jong na kutuma mpira wa kichwa uliotinga wavuni dakika ya 84.

Klaassen aliyetokea benchi alijibu upesi zaidi dakika tisa baada ya dakika za lala salama kupiga shuti lililotoka kwa Memphis Depay na kuwaweka sawa Waholanzi kileleni mwa kundi pamoja na Ecuador, ambao watakutana nao kwenye mchezo wao ujao Ijumaa.

Post a Comment

0 Comments