NA DIRAMAKINI
TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) jijini Dar es Salaam inakabiliwa na changamoto ya wachezaji sita tegemeo ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ambapo kwa sasa wanaendelea na matibabu.
Wachezaji hao ni Hance Masound ambaye aliumia jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars na hivyo kushindwa kuendelea jambo lililopelekea kukimbizwa hospitali na gari la wagonjwa.
Christina Mwagala ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano KMC ameyabainisha hayo leo Novemba 24, 2022.

Aidha,Mwagala amesema wachezaji wengine ni Kelvin Kijili, Awesu Ally Awesu pamoja na Emmanuel Mvuyekure ambao hawa pia walikuwa na majeraha ya muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kusafiri na timu kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars.
"Kwa sasa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya wachezaji wenye majeraha, na ukiangalia kwenye timu kila mchezaji ana mchango mkubwa pindi anapopewa majukumu na kocha, hivyo nikipindi kigumu lakini tutajitahidi kadiri tuwesavyo ili kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja,"amesema.