Wafanyabiashara wa madirisha,milango nchini Algeria walinyatia soko la Afrika

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI kadhaa za Algeria zilizobobea katika utengenezaji wa madirisha na milango kulingana na teknolojia ya kisasa zaidi katika sekta hiyo zitaanza kuuza bidhaa zao zinazokidhi viwango vya kimataifa kwa nchi za Kiafrika ndani ya mwaka mmoja au miwili ijayo.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki huko jijini Algiers nchini Algeria na Abdennour Ait Mahdi ambaye ni gavana wa Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Bidhaa za Madirisha na Milango (International Fair of Facades, Doors and Windows) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusu maandalizi ya maonesho hayo.

Maonesho hayo ya siku nne kwa maana ya Novemba 30 hadi Desemba 3, mwaka huu yatafanyika katika jengo la maonesho la kisasa jijini Algiers, katika ukumbi wa CIC.

"Bidhaa za Algeria zimekuwa sana, katika miaka ya hivi karibuni zimeonesha ubora wa hali ya juu zaidi ikishindana na bidhaa za kigeni zinazoagizwa kutoka nje.

"Zaidi ya kampuni 100 za Algeria na kampuni 10 za kigeni zitawasilisha teknolojia mpya zaidi za kibunifu katika utengenezaji wa milango, madirisha na madirisha ya mbele ya vioo, ambayo yanazingatia kuheshimu mazingira na uokoaji wa nishati katika sekta hii.

"Awamu ya Nnne ya Maonesho ya Kimataifa ya Facades, Doors and Windows yataanza Novemba 30 hadi Desemba 3 ijayo, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Abdellatif Rahal (Algeirs), ambacho kitashuhudia mwaka huu ongezeko la idadi ya washiriki na pia katika maonesho hayo kuna nafasi kubwa iliyotengewa, ikidhirisha kwamba tukio hili linalenga kukuza shughuli zinazohusiana na milango, madirisha na huduma nyinginezo ili kuleta teknolojia ya kisasa.

"Ni katika kukuza uchumi moja kwa moja kupitia soko la kimataifa, pamoja na kuwajulisha wataalamu na watu binafsi kuhusu umuhimu na jinsi ya kulinda mazingira, pamoja na kuhimiza uwekezaji, kuunda nafasi mpya za ajira na kuwasilisha vifaa na teknolojia za kisasa zinazotumika katika sekta hii,"amesema Abdennour Ait Mahdi.

Amesema, kando ya maonesho hayo, mihadhara na warsha za kiuchumi na kisayansi zitaandaliwa na wataalam wa Algeria na makampuni ya kimataifa ili kuanzisha utamaduni wa kitaaluma katika ufungaji wa bidhaa hizo,na nafasi itatolewa kulingana na mzungumzaji kuelezea na kufafanua umuhimu na jinsi ya kufunga madirisha na milango kwa usahihi.

Abdennour Ait Mahdi amesema, mbali na tukio hilo kujitolea kuwaleta wageni pamoja na waoneshaji wa huduma na thamani za madirisha na milango jijini Algiers ambapo yataleta pamoja zaidi ya chapa na makampuni 100 za kitaifa na kimataifa pia yanatarajiwa kukaribisha zaidi ya wageni 6,000.

Aidha, kwa mujibu wa Gavana huyo mamia ya bidhaa na bunifu zaidi zitaoneshwa kwenye eneo la mita za mraba 8000 na zaidi ya mikutano zikiwemo warsha 15 zitaandaliwa na kuongozwa na wataalamu wakati wa SIFFP 2022.

SIFFP International Fair Algiers pia inajumuisha kampuni zinazowasilisha mifumo ya pergola (mifumo thabiti ya bustani za nje), mahema na zaidi.

Abdennour Ait Mahdi amesema, pia kutakuwa na maonesho ya ufanisi kwa kutembelea waendelezaji, wasanifu, pamoja na makampuni ya ujenzi.

Wageni kama mafundi seremala na wataalamu wa ujenzi wanaalikwa kuja kujionea bidhaa bora na bunifu zinazokidhi mahitaji yote ya soko wakati wa maonesho ya siku nne.

Amesema, waoneshaji wanaalikwa kufikia maelfu ya wanunuzi waliobobea na kuwasilisha biashara na chapa zao na kupata mabadiliko bora zaidi ya bajeti yao ya uuzaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news