Wahimizeni waumini wenu kuzingatia mila, utamaduni na maadili ya Kitanzania-Rais Samia

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuwahimiza waumini wa dini zao kuzingatia mila, utamaduni na maadili ya Kitanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu mradi wa Ujenzi wa Kanisa Jipya la Waadventista wa Sabato katika eneo la Uhindini jijini Dodoma.

Rais Samia ametoa wito huo leo katika hafla ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Aidha, Rais Samia amewataka Viongozi wa dini kuendelea kuwaandaa watoto na vijana katika malezi yenye maadili na tabia njema ambayo yatawajenga kuwa wazalendo kwa nchi yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, kwenye Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Serikali inatambua mchango wa Waadventista wa Sabato katika kuelimisha jamii katika ngazi zote kuhusu masuala ya afya na maisha bora kupitia machapisho mbalimbali na vyombo vya habari.
Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa dini kuliombea taifa ili liendelee kudumu katika amani, umoja na mshikamano ambayo ndio msingi mkuu wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi, kutunza misitu pamoja na vyanzo vya maji ili tabianchi irudi kuwa kama zamani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news