Watoa huduma za mawasiliano waaswa kutobadilisha gharama za vifurushi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kutobadilisha vifurushi vya vya Inteneti hadi pale watakapotoa bei elekezi Januari 2023.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 21, 2022 kuhusiana na kukamilisha wanabodi ya watumiaji na watoa huduma za inteneti nchini.
Amesema wako katika hatua za mwisho kukamilisha tathmini ya gharama za huduma za mawasiliano nchini na kwamba wanategemea kushusha gharama za vifurushi hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 21, 2022 jijni Dar es Salaam, Nape alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala wa vifurushi mbalimbali vya simu ikiwemo intaneti huku watumiaji wakihoji hatua zinazochukuliwa na serikali.
Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekuwa ikifanya tathmini kila baada ya miaka mitano na kwamba tathmini ya mwisho imefanyika mwaka 2018 huku gharama za huduma hizo zikiwa kati ya Sh 2.03 na 9.35.

"Watumiaji wa huduma wengi wameeleza kuwa hawafurahishwi na huduma za mawasiliano zinazotolewa na hakuna mawasiliano mazuri kati ya watumiaji na watoa huduma hivyo kusababisha malalamiko juu ya huduma na hatua zinazochukuliwa na serikali." Amesema Nape.

"TCRA inafanya tathmini kila baada miaka mitano na Desemba 2022 itakamilika, hivyo matokeo yatatolewa Januari kwahiyo nawaomba watoa huduma kutofanya mabadiliko yoyote ya bei za bundle (Vifurushi)katika kipindi hiki ambacho tathmini inaendelea hadi itakapokamilika."
Ameongeza kuwa katika tathmini hiyo inaangalia uwekezaji uliofanywa na kampuni za simu na kodi wanayolipa ili kuwa na bei elekezi na mategemeo yao ni kushusha gharama hizo kwa kiasi fulani.

Aidha, ameongeza siku saba kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kuomba nafasi za ujumbe wa bodi ya Baraza la Ushauri la Watumia huduma za Mawasiliano (TCRA -CCC).

Nape alisema baraza hilo limekuwepo tangu TCRA ilipoanzishwa lakini haijulikani hivyo wanalenga kuimarisha baraza hilo ili liwasaidie kutengeneza mahusiano mazuri kati ya watoa huduma na watumiaji.

Amesema baraza hilo lina majukumu ya kuwakilisha maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, kupokea na kusambaza taarifa za maoni ya wadau, kuwa na kamati ya watumiaji wa huduma ngazi za mikoa na kufanya mashauriano na wahusika katika sekta hiyo.
"Baraza lingekuwa na nguvu lingesimamia mahusiano yaliyopo kati ya watoa huduma na watumiaji lakini baraza hilo bodi yake imetetereka hivyo tumeongeza siku za maombi ili kupata wajumbe wa bodi," alisema.

Amesema jukumu la kwanza la bodi hiyo ni kukusanya maoni ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kuhusu utendaji, kanuni na sheria kisha wazipeleke kwenye wizara kwa lengo la kuhakikisha huduma za mawasiliano zinaboreshwa.

Ameeleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha linaondoa malalamiko na kutoelewana baina ya watumiaji wa huduma na watoa huduma za mawasiliano nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news