WDL,TAMICO wasaini mkataba kuboresha maslahi ya wafanyakazi mgodini

NA SAMIR SALUM

MGODI wa Almasi wa Wiliamson Diamond Limited uliopo Mwadui mkoani Shinyanga umesaini Mkataba wa Hali Bora na Chama cha Wafanyakazi Migodini (TAMICO) wenye lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude (anayefuata), Katibu Mkuu wa TAMICO (katikati) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakiwa wameshikilia Mkataba wa Hali Bora Baina ya TAMICO na WDL uliosainiwa leo Novemba 4, 2022.

Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika leo Novemba 4, 2022 katika uwanja wa michezo wa Mgodi wa Wiliamson Diamond Limited ukishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi.Sophia Mjema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude.

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Wiliamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda amesema kuwa, alikutana na wafanyakazi na kusikiliza kero zao ikiwemo kupata mikopo kupitia mabenki, kuboreshewa mikataba ya kazi kwa waliokuwa na mikataba ya muda mfupi na kuboreshewa maslahi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema akikata utepe kwa ajili ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited uliofanyika leo Ijumaa Novemba 4, 2022.

Amesema kuwa, tayari wafanyakazi wameshaanza mikopo na zaidi ya asilimia 75 ya wafanyakazi waliokuwa na mikataba maalumu imefanyiwa kazi.

Mhandisi Mwenda amesisitiza kuwa, ili kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi mgodini hapo ni wajibu kwao kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji ambao utawezesha kuboresha maisha yao, kuchangia jamii inayozunguka mgodi huo na kuchangia katika uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amewaasa wafanyakazi pamoja na Mgodi wa Wiliamson Diamond limited kuhakikisha kila upande unatekeleza wajibu wake ili kutimiza matakwa ya mkataba huo ikiwemo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wakiwa kazini, afya na kuboresha maslahi yao.

RC Mjema licha ya kuupongeza uongozi wa mgodi kwa kusaini mkataba huo amewataka uhakikisha unasajiliwa na Kamishna wa kazi ili uanze kazi mara moja huku huku akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa, weledi na kwa uaminifu ili kuongeza uzalishaji hali itakayowezesha kuboreshewa maslahi yao.

Aidha amizitaka Taasisi na makampuni yaliyopo katika Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wafanyakazi wanapewa mikataba, kuwaruhusu kujiunga na vyama vya wafanyakazi, kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wageni wanaofanya kazi kuwa na vibali maalumu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Sophia Mjema akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliyofanyika leo Ijumaa Novemba 4, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa TAMICO (katikati) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakizungumza jambo katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliofanyika leo Ijumaa Novemba 4, 2022.

Naye Katibu Mkuu wa TAMICO, Peternus Rwechungura amemshukuru Meneja Mkuu kwa kushirikiana na wafanyakazi na kusaini mkataba huo kwani ni takwa la kisheria na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na kampuni hiyo ikiwemo kufanya majadiliano na kuboresha zaidi mkataba huo.

Pia amewahimiza wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kupata haki zao, kutambuana na kunadiliana ili kuweza kupata haki zao.
Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakisaini mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited leo Ijumaa Novemba 4, 2022.
Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakionesha mikataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited baada ya kusainiwa leo Ijumaa Novemba 04, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Katibu Mkuu wa TAMICO na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond limited, Mhandisi Ayoub Mwenda wakikata keki ishara ya kukamilika utiaji saini wa mkataba wa Hali Bora ya wafanyakazi baina ya TAMICO na Mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond limited iliofanyika leo Ijumaa Novemba 4, 2022.

Awali akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema, Kaimu Katibu wa Tawi la TAMICO, katika Mgodi wa WDL, Gatti Raphael amesema kuwa hadi sasa kampuni hiyo imekuwa na mkataba wa hiari (voluntary agreement) hali iliyopelekea kuanzisha mazungumzo ya kuanzishwa mkataba huo ambao utaboresha maslahi ya wafanyakazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news