Rais Samia afanya uteuzi GBT

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Modest Jonathan Mero (Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Michezo ya Kubahatisha (GBT).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 4, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi Zhura Yunus ambapo uteuzi huo umeanza mara moja.

Balozi Mero ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya African Discovery Group, New York nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments