Yanga, Club Africain zatoshana nguvu Dar

NA DIRAMAKINI

YANGA SC yenye maskani yake maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam, Tanzania imekubali kugawana alama moja moja na Club Africain leo.
Ni kupitia mtanange wa mtoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika ambao umepigwa leo Novemba 2, 2022 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Huo, ulikuwa ni mchezo wazi kwa timu zote mbili ambazo zilikuwa kwenye msako wa ushindi kupiga hatua moja kuelekea kwenye hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.

Aidha, kete ya kwanza ya Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi imekamilisha dakika 90 za awali bila kuambulia bao ikiwa nyumbani na mashabiki wake ambao walikuwa na shauku kubwa ya kusonga mbele.

Baada ya klabu hizo kutoka suluhu ya kutofungana leo, kwa sasa kazi iliyopo mbele ni kusaka ushindi ugenini nchini Tunisia.

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa utaamua hatma ya nani atakayesonga mbele ambapo kwa leo,nyota wa Yanga, Khalid Aucho, Bernard Morrison na Fiston Mayele ni miongoni mwa wale ambao walianza kikosi cha kwanza.

Yanga SC licha ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo huo wameonesha kuhitaji ushindi kwa kucheza kandanda safi kwa kujitahidi kutafuta bao bila mafanikio.

Pia Yanga SC kwa sasa inahitaji sare yoyote ya mabao kwenye mchezo unaofuata ambao utapigwa nchini Tunisia ili aweze kufuzu hatua ya Novema 9, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news