Zanzibar ni eneo bora kwa uwekezaji-Waziri Soraga

NA MWANDISHI WETU

MABALOZI wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani wameelezwa kuwa, Zanzibar ni eneo nzuri na bora kwa uwekezaji na utashi wa kisiasa ni mkubwa kuhakikisha wawekezaji wenye dhamira ya kweli kutoka pande zote za Dunia wanahudumiwa ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe akitoa neno kuhusu uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu Zanzibar.

Hayo yamebainishwa Novemba 17, 2022 jijini Zanzibar na Waziri wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Mudrik Ramadhani Soraga wakati akizungumza na mabalozi kuhusu fursa zinazopatikana katika maeneo ya uchumi wa buluu na uwekezaji kwenye miundombinu.

Mheshimiwa Soraga amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji ikiwemo kuboresha sera za uwekezaji.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Togolany Mavura akichangia jambo kuhusu mada ya uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu.

Sambamba na kuweka kituo cha huduma kwa pamoja, vituo vya kikodi na kisheria ikiwemo kutengeneza mifumo rafiki ya huduma kwa wawekezaji, yote ikilenga kuhakikisha wawekezaji hawasumbuki.

Pia, Mheshimiwa Waziri Soraga amewahakikishia mabalozi kuwa, wawekezaji watakaowashawishi kuja nchini ambao watakuwa na mitaji na kuheshimu sheria na masharti ya nchi, Serikali itawapa huduma stahiki bila ubabaishaji.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Abdallah Possi akichangia mada kuhusu uwekezaji katka uchumi wa buluu Zanzibar.

Akizungumzia fursa za uchumi wa buluu zinazopatikana Zanzibar, Mheshimiwa Waziri Soraga ametaja kuwa ni pamoja na utalii, gesi na mafuta, bandari, miundombinu ya TEHAMA, usafirishaji na uvuvi.

Mheshimiwa Waziri Soraga amesisitiza umuhimu wa mabalozi kutafuta wawekezaji katika maeneo hayo na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Pia amesema,maeneo mengine yanayohitaji wawekezaji ni ujenzi wa bandari hususani Bandari ya Mangapwani ambayo itajumuisha ujenzi wa bandari za mizifo na makasha, uvuvi, gesi na mafuta, chelezo na mji wa kisasa.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akitoa neno kuhusu uwekezaji katika uchumi wa buluu Zanzibar.

Mheshimiwa Waziri Soranga amesema fursa nyingine katika uchumi wa buluu ni uvuvi kwenye bahari kuu, ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani bidhaa za samaki na mwani, vifaa vya kuhifadhia samaki. ununuzi wa meli kwa ajili ya mizigo na abiria pamoja na uwekezaji katika ujenzi wa majengo ya makazi na biashara.

Katika kikao hicho ambacho kitahitimishwa Novemba 21, 2022 mabalozi walipongezwa kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuvutia wawekezaji na kufanikisha makubaliano mbalimbali na mashirika ya Kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.

Mashirika na taasisi ambazo zimekuwa na utaratibu wa kutenga fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo duniani ukiwemo uchumi wa buluu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news