Argentina wafuzu hatua ya 16 bora, Poland wasonga mbele licha ya kushindwa 2-0

NA DIRAMAKINI

ALEXIS Mac Allister na Julian Alvarez wamefunga mabao katika kipindi cha pili baada ya Lionel Messi kukosa mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza na kuipeleka Argentina katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la FIFA kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Poland.

Ni kupitia mtanange wa nguvu wa Kundi C ambao umepigwa Novemba 30, 2022 katika dimba la 974 (Ras Abu Aboud Stadium) lililopo Ras Abu Aboud jijini Doha, Qatar.

Huku Argentina wakimaliza wakiwa washindi wa Kundi C, Poland nao walitinga Raundi ya 16 licha ya kupoteza. Kikosi hicho kinachoongozwa na Robert Lewandowski kiliishinda Mexico ambayo ilishinda Saudi Arabia 2-1 kwa tofauti ya mabao.

Argentina watakutana na Australia huku Poland wakimenyana na mabingwa watetezi Ufaransa katika hatua ya 16 bora.

Alexis Mac Allister alifunga bao hilo dakika ya 46 baada ya washindi mara mbili Argentina kupiga mashuti sita yaliyolenga lango kipindi cha kwanza ikiwemo penalti ya Messi dakika ya 39.

Naye Alvarez, ambaye alikuwa anaanza kwa mara ya kwanza baada ya mechi mbili za akiba kwenye Kombe hili la Dunia, alifunga bao la pili dakika ya 67 baada ya mpira kutoka kwa Enzo Fernandez, bao ambalo liliamsha shangwe nyingi dimbani hapo. Argentina walikuwa na uwezo wa kuondoka na mabao mengi zaidi katika mechi hiyo, lakini hawakufanikiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news