Cameroon waishangaza Brazil dakika ya 92, huku wakiaga mashindano

NA DIRAMAKINI

VINCENT Aboubakar alifunga kwa kichwa dakika 92 za lala salama na kuipa Cameroon ushindi mnono wa 1-0 dhidi ya Brazil kwenye Uwanja wa Lusail.

Vincent Aboubakar wa Cameroon akishangilia baada ya kufunga bao lao la kwanza. (Picha na Dylan Martinez/Reuters).

Ni kupitia mtanage ambao ulipigwa Desemba 2, 2022 nchini Qatar huku Aboubakar akitolewa nje kwa kadi ya pili ya njano kwa kuvua jezi wakati wa kusherehekea, lakini akaifanya Cameroon kuwa taifa la kwanza la Afrika kuwafunga mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia.

Kikosi cha Rigobert Song, hata hivyo kilishindwa kutinga hatua ya makundi, wakati Uswizi ilipoilaza Serbia 3-2 katika mechi ya kusisimua kwenye Uwanja wa 974 na kumaliza kama washindi wa pili katika Kundi G.

Brazil, ambao waliongoza kundi licha ya kushindwa, watacheza mechi yao ya 16 bora dhidi ya Korea Kusini siku ya Jumatatu huku Uswizi wakimenyana na Ureno siku inayofuata.

Kocha Tite, kama ilivyotarajiwa, alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Brazil kilichowapumzisha wachezaji tisa walioanza mechi iliyopita dhidi ya Uswizi kabla ya hatua ya 16 bora. Beki Eder Militao na kiungo Fred ndio wachezaji pekee waliobakiwa.

Huku Neymar akiuguza jeraha akiwa benchi, Dani Alves alikua nahodha mkongwe zaidi Brazil wa Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 39.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news