Uswizi wafuzu 16 bora baada ya kuifunga Serbia mabao 3-2

NA DIRAMAKINI

USWIZI imeishinda Serbia mabao 3-2 katika mchezo mkali wa mwisho wa Kundi G wa kufuzu hatua ya 16 mfululizo katika michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) nchini Qatar 2022.

Mtanange huo wa aina yake umepigwa Desemba 2, 2022 katika dimba la 974 lililopo Ras Abu Aboud, Doha nchini Qatar.

Xherdan Shaqiri alikuwa ameiweka Uswizi mbele dakika ya 20 kabla ya Alexander Mitrovic kusawazisha kwa kichwa dakika ya 26 baadaye.

Dusan Vlahovic aliwaweka Waserbia mbele dakika ya 35, lakini Breel Embolo alihakikisha timu zote mbili zinakwenda sare ya mapumziko na kumaliza kwa bao safi dakika ya 44.

Timu zote mbili zilienda mapumziko zikiwa na sare ya mabao mawili kwa mawili, hivyo mashabiki wakataka kufahamu kipindi cha pili mambo yatakuwa vipi.

Katika kipindi cha pili, Remo Freuler aliifungia timu ya Uswizi bao la tatu dakika ya 48 kwa maana ya dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza.

Bao hilo lilidumu hadi dakika tisini, ambapo ubao ulisoma Uswizi mabao matatu huku Wasebia wakiwa na mabao mawili.

Aidha, kwa ushindi huo Uswizi imeshikilia nafasi ya pili kwenye kundi hilo ikiwa na alama sita licha ya Cameroon kuwalaza Brazil kwa bao pekee. Sasa Uswizi watamenyana na vinara wa Kundi H ambao ni Ureno katika raundi inayofuata.

Remo Freuler wa Uswizi akishangilia kufunga bao la tatu akiwa na Granit Xhaka, Ardon Jashari na wachezaji wenzake wakati wa mechi ya mwisho ya Kundi G ya Kombe la Dunia la Qatar kati ya Uswizi na Serbia Uwanja wa 974 mnamo Desemba 2, 2022. (Picha na Hannah Mckay/Reuters).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news