Hizi hapa bei za mafuta kwa mwezi Desemba, 2022 nchini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus Lumato amesema, bei hizo zimeanza kutumika kuanzia leo Desemba 7, 2022 saa 6:01 usiku.

Katika mwezi Desemba 2022 bei ya mafuta ya rejareja ya petroli kwa Dar es Salaam na Mtwara imepungua kwa shilingi 59/lita na 92/lita, mtawalia, ikilinganishwa na bei za Novemba 2022, wakati bei ya Tanga imeongezeka kwa shilingi 9/lita.

Aidha,bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam haina ruzuku.Bei za rejareja za dizeli kwa Dar es salaam, Tanga na Mtwara zingeongezeka kwa shilingi 278/lita, shilingi 422/lita na 416/lita, mtawalia.

Hata hivyo, ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei za mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Mhandisi Modestus Lumato amesema, Serikali imetoa ruzuku kwa bei za Desemba 2022.

Kutokana na ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya dizeli imepungua kwa shilingi 83/lita, shilingi 247/lita na shilingi 243/lita kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, mtawalia kama inavyooneshwa katika jedwali hapa chini:

Bei za rejareja zisizo na zenye ruzuku kwa Desemba 2022 (Shilingi/Lita)
Bei bila Ruzuku

Kutokana na mgawanyo wa ruzuku kwa mafuta ya petroli na dizeli, Jedwali hapa chini linaonesha ulinganisho kati ya bei zenye ruzuku za Novemba 2022 na bei zenye ruzuku za Desemba 2022

Bei kikomo za rejareja za Desemba 2022 ukilinganisha na Bei kikomo za rejareja za Novemba 2022

Hivyo, bei kikomo za mafuta kuanzia tarehe 7 Desemba 2022 ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali hapa chini. Kutokana na bei hizi, bei za miji, wilaya na mikoani ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali linalofuata. Totauti ya bei kutoka sehemu moja kwenda nyingine inatokana na tofauti ya bandari mafuta yanapochukuliwa na gharama ya usafirishaji.

Bei kikomo za mafuta kwa kila bandari zitakazoanza kutumika kuanzia tarehe 2 Desemba 2022 (Shilingi/Lita)
Katika kutekeleza bei hizi, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia yafuatayo: -

(a) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166,bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko.

EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.

(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

(e) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina lakituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.

(f) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na.4. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara
yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

(g) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 5. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

JEDWALI NA.4:BEI ZA REJAREJA (Shilingi/Lita)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news