JIANDAENI KUMPOKEA MKOMBOZI

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa mashaka ambayo Yosefu alikuwa anayapata hata anaamua na anafikiria kumuacha Mama Bikiria Maria yalikuwa yanabatilisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika ukoo wa Daudi, kitendo hiki kitumike kwa Wakristo wote kujitafakari katika maisha yao ya kila siku.

Hayo yamesemwa katika misa ya Jumapili ya nne ya majalio leo Desemba 18, 2022 katika misa ya kwanza katika kanisa la Bikira Maria Imakuala, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

“Tujitafakari mimi na wewe tumejiandaa vipi ili huyu mkombozi azaliwe katika maisha yako? Maisha tunayoishi inawezekana wewe ni baba wa familia, yawezekana wewe ni mama wa familia, yawezekana wewe ni mtoto au pengine wewe ni kiongozi pengine katika kanisa, pengine ni kiongozi katika jamii na pengine ni kiongozi katika serikali, jitafakari unaishi vipi na wale wanaokuzunguka?.

“Unaishi vipi na watu walio chini yako? Unaonesha mshikamano pamoja na hawa watu? Unaonesha kuwa pamoja nao? Au unashindwa kutimiza wajibu wako kuwatumikia?.

“Kushindwa kuyafanya hayo unaonesha watu mashaka kama yale ya Yosefu ya kutaka kumuacha mama Bikira Maria na huko ni kuharibu mpango wa Mwenyezi Mungu kuzaliwa kwa Yesu katika ukoo wa Daudi.”

Akiyasoma maneno ya Utangulizi ya maombi ya misa hiyo, Paroko Mapalala alisema kuwa Mungu alimtayarishia mwanae makao yake hapa dunia kwa kumchagua Mtakatifu Yosefu awe Baba Mlishi wa Familia Takatifu na alimteua mama Bikira Maria awe mama wa mkombozi

“Uwajalie wakina baba na familia ukarimu wa Baba Mlishi Yosefu katika kuyaangalia mahitaji ya familia zao Ee Bwana.” Hilo likiwa mojawapo ya maombi ya misa hiyo.

Mpaka misa hii ya kwanza ya dominika ya nne ya majalio inayoanza saa 12. 00 asubuhi inamalizika mvua katika eneo la Chamwino Ikulu kwa juma zima imenyesha mara moja tu nayo miale ya jua kali ikiendelea kulishambulia eneo hili kwa ustadi mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news