Mabara yote katika raundi ya mtoano yanaonesha ukuaji wa michezo-FIFA

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limesema kuwa, Kombe la Dunia la Qatar 2022 limeweka rekodi huku timu kutoka mabara yote zikifuzu kwa hatua ya 16 kwa mara ya kwanza kabisa.

Mkuu wa Maendeleo ya Soka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Arsene Wenger. (Picha na Reuters).

Michuano hiyo iliyohitimisha hatua yake ya makundi siku ya Ijumaa iliweka rekodi kwa Shirikisho la Soka la Asia, huku timu tatu (Australia, Japan na Korea Kusini) zikifuzu hatua ya mtoano.

Timu mbili za Afrika, Senegal na Morocco, pia zinawakilishwa katika hatua ya mtoano kwa mara ya pili. Katika Kombe la Dunia la Brazil 2014, Algeria na Nigeria zilifika hatua ya 16 bora.

"Matokeo ya hatua ya makundi yanaonesha kiwango ambacho nchi nyingi zimepata zana za kushindana katika kiwango cha juu," Mkuu wa Maendeleo ya Soka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Arsene Wenger alisema Jumamosi mjini Doha na kuongeza kuwa,

“Haya ni matokeo ya maandalizi na uchambuzi bora wa wapinzani, jambo ambalo pia ni taswira ya upatikanaji sawa wa teknolojia.Mafanikio haya, yanaendana sana na juhudi za FIFA kuongeza ushindani wa soka duniani kote,"amefafanua Wenger.

FIFA pia ilisema kulikuwa na mahudhurio ya jumla ya zaidi ya watazamaji milioni 2.45 (asilimia 96) kwa mechi 48 za kwanza, ikiwa ni ya pili kwa ukubwa baada ya mashindano ya 1994 nchini Marekani.

Michuano hiyo pia ilishuhudia idadi kubwa ya watu waliohudhuria katika mchezo tangu fainali ya 1994, ambapo mashabiki 88,966 walishuhudia Argentina ikiichapa Mexico mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Lusail.

Fainali ya Kombe la Dunia ya 1994 kati ya Brazil na Italia ilikuwa na watazamaji 94,194 kwenye Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena, Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news