MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Regina Lowassa mke wa Waziri Mkuu Mstaafu (wa tatu kushoto) na Fredrick Lowassa (kulia) alipoenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa anayepata matibabu jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, Desemba 28, 2022. Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na kushoto ni  Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo Jumatano, Desemba 28, 2022 jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news